Rfi Kiswahili public
[search 0]
More

Download the App!

show episodes
 
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
 
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
 
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
 
Huu ni wasaa wa kukutana na wageni mbalimbali watakaokuwa wakifika katika studio zetu na kuzungumza moja kwa moja yaani LIVE. Ni mjadala wa kila Jumatano asubuhi ambao utagusa masuala muhimu yanayoibuka ndani na nje ya Bara la Afrika katika nyanja tofaut itofauti. Mjadala wa wiki ni wasaa utakaokuzungusha dunia nzima kupitia mawimbi ya RFI Kiswahili.
 
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
 
Talisman Brisé ni tamthilia ya redio inayosimulia hadithi ya mtunza bustani Kwame ambaye bosi wake Profesa Omar anatekwa nyara na watu wasiojulikana. Kwa nini Profesa Omar anatekwa nyara na watu hao? Mfanyakazi wake Kwame atafanikiwa kumuokoa Bosi wake? Fuatilia haya kwenye tamthilia ya Talisman Brise hapa rfi kila siku ya jumapili ndani ya Makala ya Changu Chako Chako Changu.
 
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.
 
Makala ambayo inakupa nafasi ya kujua masuala mbalimbali ya Muziki na Burudani. Ndani ya makala haya utapata taarifa za wanamuziki, historia zao na bila kusahau mahojiano na wanamuziki mbalimbali. Hii ni fursa ya pekee kwa wasikilizaji kujiliwaza baada ya kazi za juma zima kupitia burudani ya muziki. Makala ya muziki ijumaa pia itakuwezesha kufahamu wasanii kutoka sehemu mbalimbali duniani na kujua wanafanya nini.
 
Loading …
show series
 
Tunaangazia juu ya kituo cha wagonjwa wa ukoma na vikongwe kilichoko Kolandoto, mkoani Shinyanga, Tanzania. RFI imefika kituo cha Kolandoto ambapo kituo hicho kilichojengwa mwaka 1914 maalumu kwa wagonjwa wa Ukoma, leo hii kituo hicho kimegeuka kimbilio la vikongwe wanaotuhumiwa kwa uchawi ili wasiuawe na jamii inayowazunguka.…
 
Makala ya Habari rafiki jumanne hii january 25 mwaka 2022 imeangazia hatua ya wanajeshi nchini Burkina Faso kuipindua serikali ya Rais Roch Marc Chriastian Kabore wakifunga mipaka ya Nchi na makataa ya watu kutembea usiku kwa kile walichodai kiongozi huyo alishindwa kusimamia usalama wa taifaBy RFI Kiswahili
 
Makala ya juma hili imeangazia hatua ya mahakama moja kule DRC iliwahukumu kifungo cha miaka 15 jela kwa makosa ya kuwabaka wanawake wafungwa katika jela kuu la Kasapa kwenye mji wa Lubumbashi jimboni Katanga mashariki ya nchi hiyo. Uhaba wa mafuta nchini Uganda waisababishia serikali kuondoa marufuku upimaji na malipo ya lazima ya Covid-19 kwa mad…
 
Tunaangazia joto la kisiasa, linaloendelea kupanda nchini Kenya, kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Agosti mwaka huu. Wakenya watamchagua rais wao wa tano, baada ya Uhuru Kenyatta ambaye anaondoka madarakani.Kinyanganyiro kinatarajiwa kuwa kati ya kiongozi wa muda mrefu wa upinzani na aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga na naibu rais William Ruto.…
 
Tunaangazia faida za kiafya za wanaume kupashwa tohara .Kenya mwaka 2008 ilizindua kampeni ya kuwatahiri kwa khiari wanaume kuanzia umri wa miaka 15 hii ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na msambao wa virusi vya Hiv katika jamii ambazo huwa hawatahiri. Nchini Rwanda pia ambapo raia wengi hawakuunga mkono tohara ,imeanza kupata mwitikio mkubwa w…
 
Mamilioni ya wanafunzi walirejea shuleni kuanzia jumatatu ya January 10, baada ya shule kufungwa nchini Uganda kwa karibu miaka miwili, baada ya kuzuka kwa janga la Covid 19, ikiwa ndio nchi pekee duniani ambayo wanafunzi walikuwa hawajaanza masomo, kiongozi wa waasi wa ADF alikamatwa mpaka wa DRC na Burundi wiki hii, pamoja na mengine mengi. Kusik…
 
Makala hii imeangazia hatua ya spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai kujiuzulu nafasi hiyo.akisema amemuandikia barua katibu mkuu wa chama cha mapinduzi kujiuzulu nafasi hiyo, uamuzi ambao ameongeza kuwa ameufanya kwa hiari, pamoja na mapigano yanayolenga kuwatokomeza waasi wa ADF huko mashariki mwa DRC pamoja na mambo mengine ni miongoni mwa yali…
 
Viongozi wa jumuiya ya nchi za Afrika magharibi ECOWAS wameiwekea vikwazo vikali vya kiuchumi nchi ya Mali, kutokana na kucheleweshwa kwa uchaguzi kuelekea kurejeshwa kwa utawala wa kiraia.Msikilizaji, unadhani vikwazo hivyo vitaufanya uongozi wa kijeshi kubadili msimamo wake ?Unafikiri vikwazo hivyo vitawaathiri zaidi wananchi kuliko viongozi wa k…
 
Leo tunaangazia juu ya mapambano dhidi ya biashara, unyonywaji na usafirishaji binadamu kwenye ukanda wa afrika ya mashariki. Kwa mjibu wa mtaalamu wetu Bi. Winnie Mtevu kutoka Nairobi Kenya, vitendo hivo viovu dhidi ya binadamu vinafanywa ndani na hata nje ya mipaka ya nchi husika, ikiwa ni kinyume kabisa na haki za binadamu.…
 
Loading …

Quick Reference Guide

Copyright 2022 | Sitemap | Privacy Policy | Terms of Service
Google login Twitter login Classic login